Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Muqtada al-Sadr, kiongozi wa Harakati ya Sadr, amelaani shambulio la kigaidi lilofanywa katika Msikiti wa Imamu Ali (a.s.) katika mji wa Homs nchini Syria, na kuitaka serikali ya Syria mara moja kuzuia na kudhibiti misimamo mikali ya kimadhehebu, na kuiweka mbali na nguzo za serikali pamoja na uchaguzi ujao.
Matini ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa huzuni iliyochanganyika na ghadhabu kubwa, tumepokea habari ya kulipuliwa Msikiti wa Imamu Ali (a.s.) – ambao umepewa jina la binamu wa Mtume (s.a.w.w.) na wasii wake – katika nchi pendwa ya Syria.
Aliongeza kusema: ubaguzi wa kimadhehebu ni fedheha, na mauaji ya Alawi na Ahlus-Sunna hayana uhusiano wowote na serikali iliyoangushwa!!! Kwa mtazamo wangu, kitendo hiki ni tangazo la kuanza kwa vita vya kimadhehebu ambavyo Iraq yetu pendwa ilishawahi kuteseka navyo hapo awali; hivyo basi, tunaishauri serikali, mara moja kudhibiti misimamo mikali ya kimadhehebu na kuiweka mbali na mihimili ya dola pamoja na uchaguzi ujao.
Muqtada al-Sadr alifafanua kuwa: Watu hawa wajue kwamba; kulipua msikiti au hekalu ni kuivunjia heshima sehemu ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu, lakini kuvunjwa heshima ya damu ya mwanadamu, kunakodhalilishwa na watu waliopotea ni kosa kubwa zaidi; kinyume na alivyosema mola na bwana wetu Imamu Ali, Amirul-Mu’minina (a.s.):
«(الناس) صنفان إما أخ لك في الدين أو نظير لك في الخلق»(Watu wako katika makundi mawili: ima ni ndugu yako katika dini, au ni sawa na wewe katika uumbaji).
Kwa msingi huo tunaelewa kuwa; si maadui na si marafiki zetu miongoni mwa Ahlus-Sunna pekee wanaomwaga damu, bali kila mwanadamu, dini yoyote aliyonayo, ikiwa si ndugu yako, basi ni sawa nawe katika uumbaji.
Kiongozi wa Harakati ya Sadr aliendelea kusema: Acha fedheha hii na upotofu huu kutoka katika Sunna ya Mtume (s.a.w.w.), ambaye hakuwajia watu kwa kuchinja na milipuko, bali alikuja kwa maadili mema na kukamilisha ukamilifu wa tabia njema… na enyi waliopotea, jueni kwamba… ninyi si watawala, si majaji, wala si watekelezaji wa hukumu; bali ninyi ni minyoo iliyotanda katika mwili wa ubinadamu, si Uislamu pekee, na kwa kuchochewa na adui wa pamoja – pembetatu ovu – mnatekeleza vitendo hivi. Syria pendwa ni ya madhehebu yote na si mali ya kundi fulani, wala haitasalimishwa kwa makundi ya kigaidi; bali itabaki huru na yenye heshima mbele ya dhulma, ugaidi na kuhalalisha uhusiano.
Maoni yako